MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera SACP Augustino Olomi kuwachukulia hatua askari wote wa polisi wa Wilaya ya Kyerwa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo, Justine Joseph, kwa tuhuma za kusindikiza kahawa ya magendo kwenda nchi jirani.
Hayo yameelzwa leo Jumatatu, Oktoba 8, 2018 na Msemaji wa Jeshi la polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakaluka ambaye amesema kwamba kufuatia sakata hilo, IGP Sirro amepeleka timu maalum ya kuchunguza tuhuma hizo huku akimwondoa Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Justine Joseph ili kupisha uchunguzi huo.