Rais John Magufuli amepokea hundi ya shilingi milioni 125 kutoka kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambayo iliwasilishwa na Balozi wa Kenya hapa nchini, Dkt. Dan Kazungu ikiwa ni rambirambi ya ajali ya MV Nyerere iliyotokea Septemba 20 mwaka huu, Ukerewe Mwanza.
