×

WEMA ALIVYOPANGUA KIBISHI TUHUMA ZA KULALA NA DOGO JANJA

MALKIA wa Bongo Muvi, Wema Sepetu amekanusha vikali tetezi ambazo zilizosambaa mitandaoni kwamba kuna siku alichepuka na Dogo Janja ambaye ni mume wa ndoa wa msanii mwenzake, Irene Uwoya.

 

Baada ya kuibua tetesi hizo, Wema ambaye siku ya jana alimtangaza mpenzi wake mpya, amedai sio kweli kwamba anatoka kimapenzi na mpenzi huyo wa Irene Umoya.

 

“Pale unapoona mtu anakuongelea vitu visivyo make sense ili mradi tu… Mi Arusha nimeenda Lini…??? Na Huyo Dogo nimekaa nae WAPI…???? Hata mazoea nae sina…!!!Ila Dada anakuwaga na stress za ajabu sometimes… Kimambi… Utaniacha lini nipumue in Peace…!??? You are Obsessed wallahy,” aliandika Wema Sepetu.