BAADA ya kupata taarifa ya kifo cha Nguli wa filamu nchini aliyeng’ara sana kupitia kundi la Kaole, Mzee Mashaka, Global TV jana ilifunga safari mpaka msibani ambapo ni nyumbani kwa marehemu Ilala jijini Dar na kuzungumza na mmoja kati ya manguli katika tasnia hiyo, Muhogo Mchungu, ambaye amezungumzia rafiki yake huyo.