
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’ ametaja sababu inayomfanya kutusua kwenye Muziki wa Bongo Fleva kuwa si kwa sababu ya uzuri alionao bali kazi nzuri anazowapa mashabiki wake.
Akizungumza na Risasi Vibes, Malaika alisema kuwa anajitambua kuwa yeye ni mzuri lakini anajitahidi kufanya kitu kizuri hata kama akikaa muda mrefu bila kutoa nyimbo lakini kutokana na msingi mzuri aliojiwekea tangu mwanzo hawezi kuanguka kama inavyokuwa kwa wanamuziki wengine.
“Unajua hata uwe mzuri kiasi gani kama huna bidhaa nzuri sokoni ni kazi bure lakini uzuri ni kwamba uwe mwanamuziki wa kike mrembo halafu pia uimbe nyimbo nzuri kwa mashabiki wako hapo hata uzuri wa sura yako utaonekana na kukusaidia,” alisema Malaika.
Stori: IMELDA MTEMA