×

MAMA DIAMOND AFUNGUKA ANAVYOSUBIRI HARUSI

 MAMA wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ amefunguka kuwa anasubiri kusherehekea harusi ya mwanaye huyo kwa shauku kubwa licha ya kwamba hajui ataoa lini na mwanamke gani’

 

Akizungumza na Risasi Vibes, mama Diamond alisema licha ya kwamba Diamond ni mwanaye, lakini hawezi kumchagulia mwanamke wa kuoa kwani hata yeye hakuchaguliwa mwanaume wa kuwa naye hivyo kikubwa anachosubiri ni kusherehekea tu siku hiyo.

“Unajua siwezi kumchagulia Diamond  mwanamke wa kuoa bali yeye mwenyewe ndiye atakayechagua maana hata kama watu wanavyosema amuoe Zari (mzazi mwenza wa Diamond) wakati wanakutana na kuanzisha uhusiano wao mpaka wakapata watoto mimi sikuwepo hivyo mambo ya kuoa ni uamuzi wa mtu mwenyewe,” alisema mama Diamond.

Stori: GLADNESS MALLYA

Mama Mzazi wa Isaac Gamba: Sitomsahau Mwanangu