×

Mb Dogg Akerwa na Mitambo

WAKATI video chafu zinazomhusu msanii wa Bongo Muvi, Wema Sepetu na video vixen, Amber Rutty zikiwa gumzo kila kona, mkongwe kunako gemu ya Bongo Fleva, Mbwana Mohamed ‘Mb Dogg’ amechukizwa na mitandao na kusema ndiyo imefanya wasanii kuharibikiwa.

 

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Mb Dogg alisema anashukuru viongozi wamekuwa macho na kuchukua hatua lakini anachukia mitandao kwani imefanya watu wengi kuiga kwa kila wanachokiona.

 

“Sisi watu weusi tuna njia zetu za kuishi sasa mitandao imetuletea ugeni na sisi hatuwezi kutumia, tukiona mtu fulani kafanya hivi basi tunaiga,” alisema Mb Dogg.

 

Mkali huyo aliyewahi kubamba na ngoma kibao kama vile Latifa, Waja, Mapenzi Kitu Gani, Natamani na Inamaana aliongeza kuwa, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) linapaswa kukaza zaidi kwa wasanii.

 

“Basata watoe misingi vizuri, walianza na video ambazo zamani ilikuwa mguu ukionekana sawa lakini ukizidisha inawekwa kapuni, wakikaza kwa kutoa elimu kwa wasanii zaidi tunaweza kukaa kwenye laini vizuri na matukio kama haya yasitokee tena.”

 

 

 

 

Stori: Mikito Nusunusu