×

AY AUCHAMBUA MUZIKI WA BONGO WA SASA

AY akianya mahojiano na mwandishi, Neema Adrian.

MSANII wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘AY’ leo Jumatano, Novemba 14, 2018 amefanya ziara ndani ya mjengo wa Global Group kunapopatikana ofisi za magazeti na Global TV na kupata nafasi ya kuzungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo kisha kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya. 

AY akiwa na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.

 

Akizungumzia muziki wa sasa wa Tanzania, AY ambaye ni miongoni mwa wasanii waliyofanya kazi kubwa kuupaisha muziki wa Bongo kwenda Kimataifa, amesema muziki huo umekua mkubwa kwani hapo zamani waliyokuwa wakinufaika ni mapromota huku wasanii wakiambulia patupu.

AY akiwa ndani ya Studio za Global TV Online na mtangazaji Lukas Masungwa.

“Kwa sasa hivi wasanii wetu wanawezakutoka hapa kwetu na kwenda kufanya shoo nje ya nchi mfano Kenya, wanafanya matamasha makubwa ya ndani na nje, wanalipwa posho zao vizuri, maisha yao unayaona yanabadilika tofauti na hapo awali. Naona kabisa muziki wetu umetanuka na tukiongeza bidii, juhudi na ubunifu zaidi tutafika mbali,” alisema AY.

AY katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi na wahariri wa Global Publishers baada ya kumaliza kuzungumza nao.

Akiwa hapo aliweza kubadilisha uzoefu wa kiburudani na wahariri wa Magazeti Pendwa ya Risasi, Amani, Ijumaa na Uwazi kisha pia akabadilishana mawazo na wahariri wa magazeti ya michezo, Championi na Spoti Xtra kisha kumalizia kwa wafanyakazi wa Global TV.

 

“Niwapongeze Global Publisher, mnafanya kazi kubwa ya kuhabarisha umma wa Watanzania, mnaburudisha na mnaisaidia jamii, hongereni sana,” alisema AY.

Kwa mahojiano exclusive na AY, usikose kufuatilia Gazeti la Ijumaa kesho na Gazeti la Spoti Xtra, Jumapili hii.

 

Na Neema Adrian, Global Publishers.