×

Kwa jero tu unashinda uzi orijino wa Simba na Yanga

WASOMAJI kibao wa Gazeti la Spoti Xtra kila Alhamisi na Jumapili watakuwa wakijishindia jezi orijino za Simba na Yanga zenye logo ya SportPesa kwa kununua gazeti hili kwa jero tu.

 

Jezi hizo ni za rangi mbalimbali za klabu hizo na msomaji au shabiki wa Simba na Yanga atakuwa anachagua mwenyewe rangi anayoitaka na saizi inayomfaa.

Mhariri Mtendaji wa Global Group, Saleh Ally ‘Saleh Jembe’ alisema huo ni muendelezo wa zawadi baada ya zile jezi za Ulaya ambazo zimekuwa zikitolewa kila wiki.

 

“Ni rahisi sana kuendelea kujishindia hizo jezi orijino, msomaji anunue tu gazeti kwenye ukurasa wa pili kuna maelekezo rahisi kabisa ya kushiriki na droo ni ya wazi kabisa na watu kibao wanashinda kila wiki,” alisema Saleh ambaye ni mchambuzi nguli zaidi nchini na mmiliki wa Blog ya Saleh Jembe.

 

“Jezi orijino zipo nyingi sana tumeagiza mzigo wa kutosha na za Ulaya pia zipo stoo za kutosha ndio maana msomaji au shabiki akishinda hapohapo anakuja kuchukua kwenye ofisi zetu za hapa Sinza, Mori,” aliongeza Saleh.

 

Alifafanua kwamba kwa wasomaji wa mikoani wamekuwa wakipata jezi zao kwa utaratibu maalum kuepuka usumbufu na ziwafikie kwa wakati hivyo wasijali waendelee kushiriki kwa nguvu zote kwa kununua Spoti Xtra kwa jero tu.

MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM