




Wabunge na viongozi wa Serikali, jana walikuwa ni sehemu ya burudani ya aina yake katika Tamasha kubwa la muziki la Tigo Fiesta 2018, lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.
Tamasha hilo lilifanikiwa kuwavuta mashabiki wa muziki wa bongo fleva kutoka mkoa huo na viunga vyake, lilianza kwa msanii Jay Melody kupanda jukwaani na kutoa burudani safi ‘iliyobamba’na kutengeneza mazingira safi kwa waliomfuatia.
Baada ya wasanii kadhaa kupanda jukwaani, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi alipanda jukwaani kuzungumza jambo kabla ya kuomba kuwekewa muziki wa bolingo na kucheza mwanzo mwisho na kuamsha shangwe za ktosha kwa mashabiki.
Wakati Katambi akiendelea kusakata bolingo, baadhi ya wabunge wakiongozwa na mbunge wa Sengerema William Ngeleja waliomba kuwekewa muziki wa Kwaito ambao waliusakata kwa ufundi mkubwa na kusababisha shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki.
Wasanii wanaounda kundi la Weusi, Bill Nas, Barnaba, Rosaree ni baadhi ya ambao wataendelea kukumbukwa na wakazi wa Dodoma kutokana na kutoa burudani safi kwa wakazi hao ambao walionekana kuwa na kiu ya burudani.
Ili kunogesha msimu wa Tigo Fiesta 2018, kampuni ya simu za Simu za mkononi ya Tigo imewaletea promosheni bab-kubwa inayojulikana kama Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. ‘Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Uthman Madati alisema katika tamasha la Mwanza.
Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia. Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.