
Rapa wa Atlanta, Marekani aliyefanya vizuri na wimbo wake wa Kiss Me Thru The Phone mwaka 2008, SOULJA BOY ametangaza kusaini dili jipya na Lebo ya Entertainment One.
Ijumaa Novemba 16, kupitia akaunti yake wa Twitter aliandika, “Rasmi nimesajiliwa na eOneMusicUs, shukrani kwa mashabiki zangu wote, naahidi kuachia muziki mpya na kufanya kazi kwa bidii.”

Posti hiyo ilifuatiwa na posti nyingine katika ukurasa wake wa Instagram yenye picha ikimwonyesha akisaini mkataba huo.

SODMG ndiyo lebo ambayo ilikuwa inammiliki msanii huyo kabla ya kusajiliwa kwenye Entertainment One.
- ISIKUPITE:“Diamond Ana Mapungufu / Tunavumilia / Alikiba Kudhamini..”Lava Lava