NJEMBA mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, amejikuta akinyukwa na kuangukia mikononi mwa polisi baada ya kudaiwa kufanya vurugu katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo limejiri leo Ijumaa, Novemba 23, 2018 mara baada ya njemba huyo kuonekana akigombana na askari polisi waliyokuwepo katika eneo hilo la Mahakama wakati kesi zikiendelea.
Global TV Online imefanikiwa kunasa picha na video za tukio zima huku polisi hao wakimchukua na kudai wanakwenda kumfungulia kesi kwa kusababisha vurugu mahakamani.