
Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), David Kikambako (mwenye jezi ya kijani) akiwaongoza wachezaji wake kusalimiana na timu pinzani ya Kumbukumbu FC kabla ya kuanza kwa mechi ya ligi ya daraja tatu kwa Wilaya ya Kinondoni iliyopigwa jana katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jijini Dar es salaam. 
Kocha msaidizi wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Kambi Mzee Kambi akizungumza na wachezaji wake
Kocha msaidizi wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Kambi Mzee Kambi akiongoza dua kabla ya mechi
Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Hussein Khamis akiwania mpira na mchezaji wa Kumbukumbu FC, Shauri Abbas

Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Hussein Juma akiwania mpira na mchezaji wa Kumbukumbu FC, Musa John wakati wa mechi hiyo ikiendelea

Mzee Kambi akizungumza na wachezaji wake wakati wa mapumziko katika mechi ya ligi ya daraja la tatu kwa wilaya ya Kinondoni iliyopigwa katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jana jijini Dar es salaam. DTB iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kumbukumbu FC. Kulia ni Kocha mkuu wa timu ya hiyo, Michael Lugalela.