


BENKI ya NBC imetoa ofa ya kuwafadhili wanafunzi wa Kitanzania kusomea shahada ya kwanza katika vyuo vya CBE, IFM, DUCE, na Chuo cha Wanyamapori MWEKA, ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuchangia sekta ya elimu nchini Tanzania. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi wakati akizungumza na wahariri wa habari za biashara na Uchumi, Jumatatu ya Desemba 3, 2018, katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.
Aidha Sabi amesema benki hiyo, pamoja na mambo mengine, imedhamiria kuboresha huduma zake za kibenki kwa kuwafuata wateja popote walipo badala ya wao kuwafuata.