Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Faustine Ndugulile (kulia) akikabidhiwa viti na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam (wapili kushoto), Badru Idd katika hafla ilyofanyika Hospitali ya Taifa, Muhimbili.
SERIKALI kupitia kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Faustine Ndugulile imezuia Televisoni (TV) zilizopo kwenye vituo vya afya na hospitali kuonyesha muziki, filamu, soka pamoja na michezo mingine na badala yake zinapaswa konyeshe vipindi vya kuelimisha kuhusiana na afya.
Ndungulileameyasema hayo jana alipokuwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupokea msaada wa viti kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya matumizi ya mapokezi ya hospitali hiyo.

Viti hivyo ambavyo vina uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 200 thamani yake ni Shmilioni 10.
“Uamuzi huo tuliufikia hivi karibuni kwa hiyo tunaziomba hospitali nyingine ambazo bado hazijaanza utaratibu huu kuuanza mara moja.”
“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa TV hizo zinatumika kwa ajili ya kutoa elimu ya afya kwa watu wote wanaofika hospitali na siyo kitu kingine,” alisema Ndungulile.