
Rapa Cameron Jibril Thomaz maarufu kama Wiz Khalifa amekataa kwamba yeye ni mfalme wa muziki aina ya R&B na kumpa msanii mwingine tofauti ambaye watu hawakudhani kama Wiz angempa hizo credit.
Kupitia mahojiano na kituo kimoja cha radio cha Power 106 FM aliulizwa “kama ukitaka kumtaja mfalme wa muziki wa R&B utamtaja nani”? ambapo Wiz alijibu na kusema kwamba, “kwa hiki kipindi chetu ni Chris Brown”

Wiz Khalifa pia ameongelea project zake za mwaka 2019 na amesema kwamba anategemea kufanya kazi na Currency ambaye ni rafiki yake wanategemea kuileta project ambayo inakwenda kwa jina la 2009 na mwakani ni lazima ataachia album pia.
Tazama Akifunguka