×

ZARI AFUNGUKA MAZITO KWA MWAKA 2018

 

Zari  The Boss Lady mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameandika mambo makubwa kwa jinsi alivyopitia katika miaka miwili iliyopita 2017 na 2018 na kusema yuko tayari kwa ajili ya 2019.

 

Kupitia akaunti yake ya  Instagram amefunguka na kueleza matatizo yote yaliyomkuba mwaka 2017 ikiwemo kuondokewa na Mama yake mzazi pamoja na aliyekuwa mume wake Ivan.

 

Pia ameeleza jinsi alivyoutumia mwaka 2018 katika kujenga na kuyarekebisha baadhi ya makosa yake na matatizo aliyopitia pia kujijenga zaidi baada ya kuondokea na wapendwa wake hao wawili na kufunguka kuwa yuko tayari kwa mwaka 2019.

 

“Mwaka 2019 niko tayari kwa mwanzo mpya. Katika maisha, sisi huumiza, tunafanya makosa, tunasamehe, tunaendelea. Lakini, zaidi ya yote na kwa njia yote tunayojifunza. Asante 2018, bado nina pumua. Shiriki nami hadithi yako ya maisha kwa mwaka 2018”.Ameandika Zari