‘TUNAFUNGA JUMLA-JUMLA 2018’: ROSTAM, MAUA SAMA WAAHIDI SAPRAIZ DAR LIVE
Global Publishers December 28, 2018
SHARE THIS:
Wasanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki (kushoto) Stamina (kulia) na mwanadada, Maua Sama wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo juu ya shoo yao ya ‘Kufunga Mwaka Jumla-Jumla’ Dar Live katika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar.Roma akizungumzia shoo hiyo na kuahidi sapraiz kibao.Stamina akiahidi kutowaangusha mashabiki watakaoingia ndani ya Dar Live usiku wa Mwaka Mpya Desemba 31 wiki ijayo.Maua Sama ambaye anatamba na ngoma ya ‘Iokote’ akiahidi kuangusha bonge la shoo ndani ya kiwanja hicho.Wanahabari wakiendelea kufanya yao.Wasanii hao wakiwa na Meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta almaarufu KP Mjomba (kushoto) na DJ Choka (kulia) ambaye anatarajiwa kuwa upande wa mitambo siku hiyo.
WASANII wanaounda kundi la Rostam, ambao ni Roma Mkatoliki, Stamina na Maua Sama, leo wamewathibitishia wapenzi wa burudani kufanya shoo ya nguvu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar usiku wa kuamkia mwaka mpya 2019.
Nyota hao ambao watapiga shoo ya pamoja, wamesema katika mkutano na wanahabari uliofanyika leo katika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar kwamba kama kawaida yao katika onyesho hilo hawataangusha mashabiki wa burudani na kuahidi sapraiz kibao za wasanii.