KUFUATIA ongezeko la vijana wengi nchini kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya hususani wasanii kutoka katika tasnia mbalimbali, Kikundi cha sanaa cha Bint Filamu kutoka Zanzibar kwa kushirikiana na wasanii wa Bongo Muvi kimeanzisha kampeni ya ‘Kataa Mihadarati’ ambapo inatoa elimu juu ya athari za matumizi ya madawa ya kulevya.

Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi Desemba 27, maeneo ya Mburahati viwanja vya barafu na kuhudhuriwa na wasanii wengi akiwemo Mtangazaji na mdau mkubwa wa filamu, Zamaradi Mketema.
Akipiga stori na Global TV katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Zamaradi amesema jamii inahitaji sana kuelimishwa kuhusiana na madhara ya madawa ya kulevya hasa wale ambao bado hawajaanza kutumia kuanzia ngazi ya shule ya msingi mpaka chuo na mitaani.

Alipoulizwa kuhusiana na hali ya Baba Watoto wake ambaye ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Zamaradi akajikuta anapata kigugumizi na kushindwa kulizungumzia hilo.