×

Tumekuwekea Hapa, Viingilio vya Simba na JS Saoura -Video

Msemaji wa klabu ya Simba SC ya Dar es salaam Haji Sunday Manara.

Simba  leo imetangaza viingilio vya mechi yao na JS Saoura ya Algeria, hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya wiki hii.

BEI YA TIKETI
MZUNGUKO 5,000
VIP B & C. 10,000
PLATINUM 100,000
Hii platinum wanapatia huduma zifuatazo:
– Watakaa sehemu ya VIP A
– Waacha gari zao Serena hotel na kuchukuliwa na Min bus maalum kuja na kurudi Taifa kwa Escout ya Police.
– Wapatewa Jezi Mpya za Simba
– Watapata bites na vinywaji wakiwa uwanjani.


HUDUMA
Siku ya Jumamosi Uwanja utakuwa wazi mapema saa 4 asubuhi na Kuanzia saa 6 hadi saa 8 kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo Twanga Pepeta Full Mziki.
Huduma ya Vyakula na Vinywaji vitakuwepo uwanjani.

TIKETI
Tiketi zinaanzwa kuuzwa Leo kwa Njia ya Selcom kwa wenye kadi wanaweza kununua Direct au kwa Mashine za Selcom.
Kuanzia Ijumaa Asubuhi mapaka Jumamosi siku ya mechi Tiketi zitapatikana kwenye Van maalim zitakazokuwepo maeneo mbalimbali maarufu wa uuzaji tiketi Posta Mpya, Kariakoo Bigbon, Karume Stadium, Uwanja wa Taifa.. Sehemu zingine zitatangazwa baadae.

JEZI

Kutokana na miutikio wa Mashindano haya Simba imetoa Punguzo la Jezi zake kuanza Leo mpaka siku ya mechi Jumamosi zitauzwa kwa 15,000 tu na zitapatikana Maduka ya Sinza na Kariakoo yanayouza Jezi zao.