Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwita waitara, ametoa onyo kwa wamiliki wa shule binafsi wanaowarudisha wanafunzi nyumbani kwa kukosa ada baada ya kupandisha ada ghafla bila ya kuwataarifu wazazi.
Naibu Waziri Waitara amesema kitendo cha kumrudisha mwanafunzi nyumbani kinamvuruga na kumvunja moyo wa kusoma tena na kutoa agizo kwa wamiliki wote wa shule binafsi kuwasiliana na wazazi kuhusu ada na sio kukurupuka na kuwarudisha nyumbani.
