×

DC MURO Afunguka Kufunga Baa ”Watu Wananywea Chooni” – VIDEO

Mkuu wa wilaya ya Meru Ndugu, Jerry Muro, ameelezea azma yake ya kuvifunga vilabu vya pombe na kurudisha uwajibikaji wa wanajamii katika shughuli za maendeleo ikiwemo uchangiaji wa Ujenzi wa Madarasa katika shule za sekondari wilayani Meru .

Suala la unywaji pombe kupita kiasi limekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wakazi wa Meru kushiriki katika Shughuli hizo hali inayopelekea Mkuu wa wilaya ya Meru kusema kuwa itafikia hatua ambayo ata vifungia kufanya kazi vilabu vya pombe vyote vilivyopo katika wilaya yake kama vitashindwa kufuata utaratibu uliowekwa wa kutofungua vilabu hivyo saa za kazi.