×

Kikwazo Ambacho Tanasha Amemwekea Diamond Kuhusu Ndoa

PAMOJA na kukaribishwa ukweni jijini Dar huku ndoa ikisubiriwa kwa shauku kubwa, ghafla tu mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni mrembo kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna Oketch amemwekea kikwazo jamaa huyo, Risasi Jumamosi linakupa zaidi.

 

Diamond au Mondi na Tanasha wanatarajiwa kufunga ndoa mwaka huu baada ya kuahirisha kufanya hivyo Februari 14 kama wawili hao walivyopanga awali. Sasa habari iliyogeuka gumzo na kuibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ni juu ya mwanadada huyo kugoma kubadili dini ili aolewe na Mondi.

 

Inafahamika kwamba, Mondi ni Muislam huku Tanasha akiwa ni Mkristo ambapo mashabiki wanaamini lazima mmoja abadili dini kumfuata mwenzake. Tanasha, akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa mashabiki kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, alisema kuwa kutokana na mipango ya ndoa inayofuata hawezi kukataa kuhamia Tanzania kwa sababu kwake kwa sasa ni nyumbani kwa pili.

 

Alisema kuwa, kuhamia kwake Tanzania haiwezi kuwa shida, lakini kwa suala la dini, hawezi kubadili dini. Tanasha alisema kuwa kila dini imekuwa ikimuamini Mungu mmoja hivyo hakuna sababu ya yeye kubadili dini zaidi ya kila mmoja kuheshimu dini ya mwingine.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, mmoja wa wanafamilia ya Mondi aliyefuatilia mjadala huo alisema kuwa, jambo hilo ni kikwazo kikubwa kwani wao kama familia walitarajia Tanasha angebadili dini ili kuungana na Mondi ambaye ni Muislam safi.

 

“Tayari hapo naona kuna shida kubwa. Sisi tulitarajia Tanasha atabadili dini, lakini naona ameanza vikwazo kwa ndugu yetu (Diamond). “Tunachojua ni kwamba, Diamond hawezi kuoa mwanamke ambaye hawatakuwa dini moja,” alisema mtu huyo aliyeomba hifadhi ya jina.

 

Risasi Jumamosi lilimtafuta Mondi ili kujua msimamo wake juu ya ishu hiyo ambapo simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa meseji kwa WhatsApp hakujibu. Ndoa ya Mondi na Tanasha imekuwa ikipingwa vikali kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mzazi mwenza wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ana vigezo zaidi vya kuwa mke kuliko ilivyo kwa Tanasha.

 

STORI: Sifael Paul DAR ES SALAAM

 

SPIKA ‘Ashindwa Kujizuia’ Amcharukia Mbunge Chadema “Acha Upotoshaji Wewe”

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club