
MBUNGE wa Misugwi na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, amehamishwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alipokuwa amelazwa na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Spika wa Bunge, Job Ndugai na viongozi wengine walimuaga Kitwanga jana Alhamisi, Januari 31, 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Jijini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Aidha, juzi Jumatano, Januari 30, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimjulia hali Mbunge huyo katika Hospitali ya Benjamin Dodoma.
