×

CHADEMA Wacharuka “Mnaua Watu, Watoto wa Mbowe Wamepigwa” – Video

BARAZA la Vijana wa Chadema BAVICHA, limetoa malalamiko dhidi ya vitendo vya jeshi la polisi nchini vinavyoingilia Uhuru wa Mahakama.

 

Akizungumza na wahandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Patrick ole Sosopi amesema Desemba 12, mwaka jana baraza hilo lilituma barua kwa Jaji Mkuu, juu ya matendo mbalimbali ambayo yanakiuka sheria za nchi, utawala wa sheria na kuingilia uhuru wa mahakama na haki za binadamu lakini amedai hawakujibiwa.

 

Aidha Sosopi ametumia fursa hiyo kumuomba Jaji Mkuu, Profrsa Ibrahim Juma kujibu barua hiyo.

 

Hata hivyo, Sosopi amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wanaotoa matamko ya kutaka kupigwa kwa mbunge wa Singida mashariki Tundu lissu kwa kuonekana yupo kinyume na serikali ya jamuhuri ya Tanzania.

VIDEO: MSIKIE OLE SOSOPI