
Wasanii wa filamu za maigizo ambao michezo yao inarushwa na luninga ya Globa TV, Sango Johanes na Rhoida Richard ambao juzi (Jumamosi) walikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wakiwania tuzo za SZIFF wameahidi makubwa baada ya kubwagwa kwenye tuzo hizo.
Wasanii hao waliingia kwenye kinyang’anyiro hicho kupitia filamu ya ardhi ya damu ambapo Sango alikuwa akiwania tuzo ya msanii bora wa kiume iliyokwenda kwa Rashid Msigalla wa Iringa. Rhoida yeye alikuwa akiwania tuzo ya msanii bora wa kike ambayo nayo ilielekea Iringa kwa mtoto Frola Kihombo anayetoka pamoja na aliyetwaa tuzo ya msanii bora wa kiume.

Kufuatia matokeo hayo wasanii hao walioiwakilisha Global TV kupitia filamu yao ya Ardhi ya damu walisema wanamshukuru Mungu kwa kuingia kwenye kinyang’anyiro kwa mara ya kwanza licha ya kukosa tuzo hizo. Sango alisema; “Mimi nawapongeza hawa madogo waliochukua hizo tuzo lakini hata mimi napata nguvu ya kufanya vizuri katika filamu zangu zijazo ili niweze kutwaa tuzo kipindi kinachofuata”. Alisema msanii huyo.
Rhoida kwa upande wake alisema; Sanaa ya filamu za Bongo imeshabadilika ndiyo maana mashabiki wengi wa filamu wanashindwa kuamini wanapoona tuzo zinaenda kwa wasanii wasiokuwa na majina makubwa mimi kwa apande nayakubali matokeo kiroho safi nami ntaongeza juhudi ili zikitolewa tuzo nyingine nami niweze kuibuka mshindi.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL