
Msanii wa kike wa muziki wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ameweka historia Jumamosi ya Februari 23, 2019 kwenye kumbukumbu za wapenda burudani wengi, achana na namna waigizaji wachanga walivyowaangusha mastaa kwenye kipengele cha Muigizaji bora wa kike na wakiume, bali namna shoo kali kutoka kwa msanii Rubby alikonga nyoyo za mamia waliofika kuhudhuria hafla hiyo ya kipekee kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini.

Rubby ambaye alipanda kwenye jukwaa la SZIFF saa 4:50 hadi saa 5:13 usiku aliamsha shangwe la maana baada ya kutoa burudani ambayo haikuacha chembe yoyote ya shaka, achilia mbali vazi lake kali.
Mbali na Rubby wasanii wengine waliotumbuiza ni Mbosso kutoka kundi la WCB ambaye aliipeperusha vyema bendera ya Wasafi kwa kutumbuza muziki wa ‘live’ na wasanii wengine.

