×

LeBron James Aipita Rekodi ya Jordan

LEBRON James ameifikia na kuipita rekodi ya nguli wa kikapu Michael Jordan katika kufunga pointi nyingi
kwenye Ligi ya NBA, sasa James anashika nafasi ya nne akiwa nyuma ya Kobe Bryant, Karl Malone na Kareem AbdulJabbar.

James alifunga pointi 31, jana na kufikisha jumla ya pointi 32,311 alizofunga tangu aanze kucheza ligi hiyo, akimpita Jordan ambaye ana pointi 32,292, lakini hiyo haikumsaidia kuiongoza Los Angeles Lakers kupata kipigo dhidi ya Denver Nuggets kwa pointi 115-99.

 

Baada ya kuweka rekodi hiyo, James alipongezwa na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa Staples Center, alipoulizwa alisema: “Kutoka kuwa mtoto wa Akron, Ohio, nilihitaji hamasa kutoka kwa MJ (Jordan) kuwa hapa nilipo.”