×

JPM AMTEUA NDUNGURU KUWA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Sera.

 

Bwana Nduguru amateuliwa kushika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango(Sera) iliyokuwa wazi

 

Kabla ya uteuzi huo Bw. Ndunguru alikuwa Naibu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)

Kufuatia uteuzi huo Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Msafiri Lameck Mbibo kuwa Naibu Kamishina wa TRA

Uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja leo Tarehe 31/3/2019