KAMPUNI ya Global Publishers, imetambulisha rasmi huduma mpya ya kupata nafasi za kazi kwa kutumia simu yako ya mkononi, mahali popote ulipo na kwa wakati wowote ili kumrahisishia mtu anayetafuta ajira kupata taarifa zote kwa urahisi.
Akizungumza na gazeti hili, Meneja wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho amesema huduma hiyo itawarahisishia kazi wahitimu wa vyuo na watu wote wanaotafuta ajira, kupata taarifa zote za ajira mpya mara zinapotangazwa kwa kutumia simu.
“Kumekuwa na changamoto kubwa kwa watu wanaotafuta ajira kupata taarifa pindi makampuni au mashirika mbalimbali yanapotangaza ajira. Wengi wamekuwa wakihangaika kutafuta magazeti au kushinda kutwa nzima mitandaoni wakitafuta nafasi za kazi.
“Sisi tunakurahisishia maisha kwa kutumia teknolojia, tunafanya kazi kwa niaba yako ya kutafuta matangazo ya ajira mahali popote yanapotangazwa kwa haraka, kisha tunakutumia kwa meseji kupitia simu yako ya mkononi.
“Meseji utakayotumiwa, itakuwa na taarifa zote muhimu kuhusu nafasi za ajira zilizotangazwa, mwajiri, sifa na vigezo, mshahara na tarehe za mwisho za kutuma maombi, pia kutakuwa na link ambayo itakupeleka moja kwa moja kwenye tangazo husika papo hapo,” alisema Mrisho na kuongeza:
“Hii itakuondolea usumbufu wa kushinda kwenye vijiwe vya magazeti kupekua matangazo ya nafasi za kazi, au kushinda mitandaoni ukitafuta matangazo ya nafasi za kazi, kila kitu utaletewa kwenye kiganja chako kupitia simu yako ya mkononi.
Namna ya kujiunga na huduma hiyo, ni rahisi sana, unachotakiwa ni kuwa na simu janja (smart phone), kisha unaingia kwenye uwanja wa meseji, unaandika neno AJIRA kisha unatuma kwenda namna 15542 (kwa watumiaji wa Vodacom pekee).
Kujiunga ni bure na ili kuanza kupata meseji za ajira za kazi, mara mbili kwa siku, unatakiwa kuwa na salio lisilopungua shilingi 99 tu kwa siku.
STORI: MWANDISHI WETU
