×

Kinachoendelea Uwanja wa Taifa, Simba vs Mazembe (Picha +Video)

Mashabiki wa timu ya Simba wakiingia Uwanja wa Taifa.

LEO Jumamosi saa 10 jioni kwa saa za Tanzania, Simba SC itaikaribisha TP Mazembe ya DR Congo katika mchezo wake wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

…Wakiendelea kuingia Uwanjani

Mechi hii ya kwanza kabla ya marudiano Aprili 13, mwaka huu huko Lubumbashi nchini DR Congo ni muhimu sana kwa Simba kupata ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri kabla ya kurudiana.

 

Pamoja na rekodi nzuri ya Simba kwenye mechi za kimataifa hasa inapokuwa nyumbani haipaswi kuingia uwanjani kwa kujiamini sana bali wanapaswa kujipanga na kwenda uwanjani kwa mipango madhubuti.

Mashabiki wa Simba wakiingia uwanja wa Taifa wakiwa na matumaini ya ushindi.

(PICHA: NICOTRAC, GPL)