Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imemkamata na kumfikisha katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Uagizaji wa Mafuta na Gesi jijini Dar, Florensi Jonathani Mashauri ili kujibu mashtaka ya wizi, uhujumu uchumi ukiukwaji wa sheria ya mafuta juu ya ujengaji wa kituo na uuzwaji wa mafuta kwa Kampuni ya UDART.
Mbali na makosa hayo, Florensi anakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha haramu ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2.

February 11, 2019, TAKUKURU iliwafikisha mahakamani watuhumiwa wa nne katika kesi ya uhujumu uchumi namba 11 ya mwaka 2019 ambpo kesi hiyo iliwahusu viongozi wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam UDART, na wafanyabiashara ambao walishtakiwa kwa makosa ya wizi kugushi pamoja na utakatishaji.