×

Betika Lazidi Kutikisa Kila Kona

 

LIKIWA na takribani miezi miwili mtaani, gazeti la Betika limezidi kutikisa kila kona ya Tanzania kutokana na utofauti wake.

Gazeti hilo ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na imekuwa kawaida kwa timu ya maofisa masoko wa Global Publishers kuingia mtaani siku gazeti hilo linapotoka ambapo leo Jumatano timu hiyo imetembelea maeneo ya Mwenge, Morocco, Mabibo na Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Wasomaji waliokutana na timu hiyo ya maofisa masoko, waliendelea kulizungumzia gazeti hilo ambalo ni mahususi kwa masuala ya kubeti.

“Betika mbali na kutusaidia katika masuala ya kubeti,  huwa pia tunapata kufahamu ratiba za ligi mbalimbali Ulaya  hivy, tunaomba kama kuna uwezekano basi ziwepo ratiba za hapa nyumbani tuweze kufahamu zaidi.

 

“Lakini mbali na hayo yote, niwapongeze tu wale wote wanaoliandaa gazeti hili, walifikiria sana mpaka kulianzisha kwani huko nyuma hakukuwa na kitu kama hiki hapa nyumbani; wametusaidia sana,” alisema mmoja wa wasomaji hao.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, naye alisema katika gazeti hilo kuna nafasi kwa watangazaji kuleta matangazo yao ili kujitangaza.

“Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

 

“Kwa kuboresha zaidi katika Jiji la Dar es Salaam, tumesambaza maboksi maalum ambayo ndani yake kuna nakala nyingi za gazeti hilo ambapo msomaji anatakiwa kuchukua na kujipatia uhondo.

“Pia bado tunapokea matangazo, hivyo hii ni fursa ya watu ambao wanataka kutangaza nasi kuleta matangazo yao kwetu,” alisema Mgema.

 

Betika lina kurasa 20 za rangi ambapo mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.