
SIMBA jana Jumamosi ilitolewa hang’iova ya michuano ya kimataifa na kukaribishwa kwenye Ligi Kuu Bara kwa kipigo dhidi ya Kagera Sugar mjini hapa.
Mabingwa hao watetezi jana walikumbana na kipigo cha mabao 2-1 ikiwa na kikosi chake chote ndani ya Uwanja wa Kaitaba na kumuacha Kocha wa Kagera, Mecky Maxime akiwa mtu mwenye furaha kubwa kama Mwinyi Zahera wa Yanga.

Hicho ni kipigo cha pili kwa Simba msimu huu kwani awali kwenye mzunguko wa kwanza ilifungwa bao 1-0 na Mbao ndani ya Kirumba. Kassim Hamis aliifungia Kagera bao la kwanza dakika ya 17 kwa kuunganisha pasi ya Ramadhani Kapera. Bao hili liliwazindua sana wakaongeza umiliki wa mpira lakini kosa wakashindwa kutengeneza nafasi za kumaliza mchezo.

Kapera ikiwa zimesalia dakika nne kwenda mapumziko akamtungua Aishi Manula kwa mpira wa kona akiutumbukiza kwa kichwa, mabeki wa Simba wakaanza kulalamika wakidhani ameotea lakini mwamuzi akasisitiza ngoma iende kati. Simba waliingia kwa nguvu kipindi cha pili ambacho Kagera walionekana kujilinda
kulinda ushindi wao, lakini dakika ya 63, Emmanuel Okwi akawaumiza na kubeba mpira haraka kupeleka kati.

Simba walitawala mchezo huo kipindi cha pili huku John Bocco, Okwi, Claytous Chama na Meddie Kagere wakiwahenyesha wenyeji ingawa bahati haikuwa upande wa Mnyama. Matokeo ya jana yanamaanisha kwamba Simba inakuwa imecheza mechi 24 dhidi ya 32 za Yanga iliyoko kileleni ikiwa na pointi 74.

Simba inabakiwa na pointi zake 60 kwenye nafasi ya tatu, lakini kitakwimu wakishinda mechi zao zote zilizosalia bado wana nafasi ya kuishusha Yanga kileleni na kubeba ubingwa wa msimu huu ambalo ndilo lengo namba moja la Mohammed Dewji ‘