×

Waamuzi wa Mechi ya Simba-KMC wachukuliwa hatua

SHIRIKISHO la soka nchini (TFF) limewaondoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu msimu huu waamuzi watatu waliochezesha mchezo wa baina ya Simba na KMC  jana Aprili 25, 2019.

 

Waamuzi hao ni Abdallah Kambuzi, Godfrey Msakila na Consolata Lazaro, ambao wametajwa kuchezesha chini ya kiwango.

 

Katika mchezo huo mwamuzi Abdallah Kambuzi ndio alikuwa mwamuzi wa kati huku Consolata na Msakila wakiwa wasaidizi.

 

Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, ulimazika kwa Simba kushinda mabao 2-1 huku ikipata penalti mbili ambayo moja  Meddie Kagere aliikosa huku nyingine ikifungwa na John Bocco.

 

Pia kuna matukio kadhaa ambayo yalilalamikiwa ikiwa ni pamoja na madai ya KMC kunyimwa penalti.