×

Mabao ya Okwi + Bocco=Biashara

KUELEKEA katika mchezo wao wa leo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Karume, Musoma, unaambiwa mabao ya washambuliaji wawili wa Simba, Emmanuel Okwi na John Bocco ukiyajumlisha ndiyo unapata idadi ya mabao yote waliyofunga wapinzani wao Biashara United katika mechi zao zote walizocheza.

 

Katika chati ya wafungaji, mshambuliaji wa Mwadui, Salum Aiyee anaongoza akiwa sawa na
Meddie Kagere wakiwa nayo 16 huku Heritier Makambo wa Yanga akiwa nayo 15.

 

Biashara ambao wanashika nafasi ya 19 katika ligi kuu wakiwa wamecheza michezo 31, wamefanikiwa kuweza kufunga mabao 22 na kufungwa 29. Okwi mwenye mabao 10 na Bocco mwenye 12 ukijumlisha mabao yao ndiyo unapata idadi ya mabao ya Biashara.