×

VIDEO: DIAMOND HAWEZI KUKATAA KOLABO YANGU-BABA DIAMOND

BABA wa msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’, mzee Abdul Juma akiwa kwenye mahojiano na +255 Global Radio aliulizwa swali kwamba watu wengi wanataka afanye kolabo na mwanae.

Katika kujibu swali hilo Baba Diamond amesema kuwa Diamond ni kijana wake, hawezi kumkatalia kolabo kwasababu ni mwanae na anamuelewa sana. Kwahiyo mashabiki waitarajie kolabo hiyo muda wowote.