×

Betika Latetema Posta DSM

GAZETI la Betika limezidi kutikisa kila kona ya Tanzania kutokana na utofauti wake na leo timu ya maofisa masoko wa Global Publishers iliingia mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam.

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, limekuwa likitolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18.

Wasomaji kadhaa wa mitaa hiyo ya Posta, licha ya jana kuwa na changamoto ya mvua, lakini walionekana kwa wingi wakiwa na nakala ya gazeti hilo.

“Mvua haituzuii kupata nakala hii ya Gazeti la Betika kwani ni gazeti letu pendwa, sipo tayari kuona nakosa nakala yake kila linapoingia mtaani siku ya Jumatano.

“Niwapongeze tu wale wote wanaoliandaa gazeti hili, walifikiria sana mpaka kulianzisha kwani huko nyuma hakukuwa na kitu kama hiki hapa nyumbani, wametusaidia sana,” alisema mmoja wa wasomaji hao.

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, naye alisema katika gazeti hilo, kuna nafasi kwa watangazaji kuleta matangazo yao ili kujitangaza.

“Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

“Kwa kuboresha zaidi katika Jiji la Dar es Salaam, tumesambaza maboksi maalum ambayo ndani yake kuna nakala nyingi za gazeti hilo ambapo msomaji anatakiwa kuchukua na kujipatia uhondo.

Mmmoja wa wasomaji wa gazeti la Betika akilionyesha.

 

“Pia bado tunapokea matangazo, hivyo hii ni fursa ya watu ambao wanataka kutangaza nasi kuleta matangazo yao kwetu.

“Kipindi hiki cha mvua tunapambana sana kuhakikisha bidhaa yetu inawafikia wasomaji wetu kwa wakati na bila kukosa,” alisema Mgema.

Betika lina kurasa 20 za rangi ambapo mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.