
MASHINDANO makubwa ya Qur-aan Tukufu yanatarajia kufanyika Jumapili hii, Mei 19, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini hapa ambapo kutakuwepo na washiriki kutoka nchi 20 barani Afrika na pia wageni kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Akizungumza na Global Puplishers, Mkurugenzi wa Taasisi ya Al-Hikma iliyoyaandaa mashindano hayo, Sheikh Nurdeen Kishk, alisema kuwa anawakaribisha watu wote bila kujali dini kwa kuwa kuwa mtu amaruhusiwa kuja kushiriki kuona jinsi vijana walivyohifandhi Qur-aan Tukufu.

Tunawakaribisha watu wote kwa kuwa Tanzania imepata bahati ya kupata washiriki watatu ambao watashindana na washiriki 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Sheikh Kishk aliwataja vijana wa Kitanzania watakaoshiriki ambao ni Shamsuddin Hussein Ali(20), Mohammad Faiz Lardhi (19) na binti pekee Sumayya Juma Abdalah (12) ambaye anatokea Mkoa wa Pwani.
“Tumpongeze kwa kuhifadhi Qur-aan Tukufu ambayo ni juzuu 30, yenye sura 144, ana aya 6636 ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa zawadi pamoja na pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni ishirini, kwa hiyo watu wote wanakaribishwa na hamna kiingilio chochote.
“Mgeni rasmi katika shughuli hiyo ambayo itaanza kufanyika asubuhi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,” alisema sheikh huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lianiva, amesema anawahakikishia wageni wote ambao watafika katika viwanja hivo kuwa usalama upo wa kutosha na pia amewapongeza wazazi kwa kuwalea watoto katika maadili ya dini.

“Niwaombe watu wote wajitokeze kwa wingi kwa kuwa viwanja vyote ikiwemo kile cha Mkapa na cha Shamba la Bibi vitatumika siku hiyo na pia kutakuwa na screen ambazo kila mtu alipokaa atapata kuona kila kitu kinachoendelea na ninawakabidhi washiriki wetu Bendera ya Taifa kwa hiyo kwa maombi yetu washiriki wetu waweze kupeperusha vizuri ili waweze kuleta ushindi katika nchi yetu na kuwapa pongezi wazazi kwa kuwalea vyema watoto wao katika maadili ya kumjua Mungu,” alisema Felix.
Stori: Neema Adrian,Global Publishers