AMA kweli hujafa hujaumbika!, Masikini Mtoto Daniela Wilfred Kalanjo(9), mkazi wa Tabata Kinyerezi jijini Dar es salaam amejikuta akiteseka baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa mara saba kufuatia kichwa chake kujaa maji na kumsababishia ukilema wa macho.