×

Kanye, Kim, Wadaiwa Kufoji Cheti cha Kuzaliwa

WAKATI wakisherehekea kutimiza miaka mitano tangu wafunge ndoa na kubahatika kupata watoto wanne, utata umeibuka kwa mtoto wao aliyezaliwa hivi karibuni ambapo inadaiwa mwanamitindo Kim na mumewe ambaye ni rapa, Kanye West wamefoji cheti cha kuzaliwa.

 

Mtoto huyo waliyemuita Psalm wakimaanisha Zaburi ambalo ni jina linalotoka kwenye Agano la Kale katika vitabu vya dini, amezaliwa kwa njia ya kupandikiza kwa mwanamke mwingine lakini utata umeibuka ambao kwa mujibu wa cheti Kim ndiye aliyejifungua jambo ambalo siyo kweli.

 

Nyaraka zilizonaswa katika Mahakama ya Los Angeles nchini Marekani zinaonesha kuwa, Kim amejifungua mtoto huyo, Mei 9, mwaka huu kupitia daktari wake wa siku zote, Paul Crane katika Hospitali ya Cedal-Sinai iliyopo Lo Angeles.

 

Daktari huyo amehusika kuwazalisha familia ya Kardashian akiwemo, Khloé, Kourtney, Kylie na Kendall. Pia alihusika kuwazalisha mapacha wa mastaa wa muziki, Beyoncé na Jay-Z’s waitwao Rumi na Sir.

 

Hata hivyo, inaelezwa kuwa, sababu kubwa ya Kim kufoji cheti ni kutokana na kutaka mtoto wao atumike katika madili ya biashara sawa na watoto wake wengine. Kanye na Kim wamebarikiwa kuwa na watoto wanne, North, 5, Saint, 3, Chicago, 1, na Psalm.

LOS ANGELES, MAREKANI