
Wachezaji wa klabu ya Simba pamoja na mashabiki wao leo mei 29, wakitokea mkoani Morogoro wameshuka Kibaha na kujiunga na msafara wa mashabiki wao kulinadi kombe lao kwa furaha na nderemo.
Mabingwa hao wa TPL msafara wao leo umeanzia Morogoro na walipofika Kibaha Stand wachezaji walipanda kwenye gari la wazi wakiwa na kombe lao wakiwaonyesha mashabiki ambao walijitokeza barabarani.

Mashabiki wengi walijitokeza kuona namna mabingwa hao wakiwa na ubingwa wao ambao ni wa pili mfululizo kwani walitwaa pia msimu uliopita wa mwaka 2017/18.
Safari kubwa ya msafara huo iliishia makao makuu ya Simba mitaa ya Kariakoo, Msimbazi ambapo nahodha msaidizi Mohamed Tshabalala alimkabidhi kombe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.



