
Kila Juni Mosi ya kila mwaka, ni siku ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa Mwenyeheri na hatimaye kuwa Mtakatifu. Ibada hiyo hufanyika katika Kanisa la Watakatifu Mashahidi wa Uganda, Parokia ya Namugongo, Kampala nchini Uganda.

Rais Yoweri Museven aliahidi kuhudhuria kila itakaofanyika ili kuenzi mchango wa Marehemu Baba wa Taifa kwa Tanzania na Uganda na kwa Afrika nzima.


Ibada za kumuombea baba wa taifa zilianza miaka sita iliyopita. Baada ya hatua hii atatangazwa kuwa Mwenyeheri na baada ya hapo atatangazwa kuwa Mtakatifu.

