×

Rwanda, Uganda Washerehekea Eid al-Fitr Leo

WAISLAM nchini Rwanda na Uganda hii leo (Jumanne Juni 4, 2019) wanasherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr na kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

 

Waumini wa dini hiyo wakiongozwa na Mufti wao Sheikh Salim Hitimana wanatarajiwa kusali sala ya Eid katika viwanja vya Nyamirambo jijini Kigali nchini Rwanda.

 

Mufti huyo alitoa tangazo la Eid nchini humo Jumatatu jioni, sawa na Uganda ambapo Baraza Kuu la Waislamu pia lilitoa tangazo kama hilo.

 

Katika salamu zake za Eid, Mufti Hitimana amewanasihi Waislamu kuendelea kutenda mema kama walivyokuwa wakifanya katika kipindi chote cha Ramadhan.

 

Nchi nyingine barani Afrika ambazo leo ni sikukuu ya Eid ni Somalia, Ethiopia, Sierra Leone, Jamhuri ya Congo. Huku nchi yenye ushawishi mkubwa kwenye masuala ya mwezi muandamo, Saudi Arabia, pia imetangaza sikukuu ya Eid leo.