×

Vee Money: Siwezi kumzuia mtu juu ya Jux

Staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

AKIWA bado anaandamwa katika mitandao ya kijamii baada ya kudaiwa kuvunjika kwa uhusiano wake na msanii mwenzake, Juma Khalid ‘Jux’, staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema kuwa hawezi kumzuia mtu kusema chochote juu yao.

 

Akizungumza na Showbiz, Vee Money alisema kwamba hawezi kuwazuia watu kusema kile ambacho wanajisikia katika mitandao ya kijamii kwa kuwa ni kawaida kwa binadamu kuongea anachokisikia.

 

“Siku zote anayeujua ukweli ni mhusika mwenyewe. Mengi yanazungumzwa lakini kikubwa mimi naangalia kazi tu,”alisema Vee Money.

#AFCON 2019: Washindi 2 Wakabidhiwa Tiketi Kuishuhudia STARS