
KAMPUNI ya Global Education Link yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, imetangaza ofa ya kipekee kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na sita, wanaotaka kwenda kuendelea na masomo yao nje ya nchi ambapo sasa kampuni hiyo, itawasaidia kutimiza ndoto zao kwa urahisi kabisa.
Uzuri ni kwamba kampuni hiyo, inamsaidia mzazi na mwanafunzi kwa mambo karibu yote ya msingi, ikiwa ni pamoja na kutafutiwa chuo, kufanyiwa taratibu zote za kusafiri na kubwa zaidi unapewa na mkopo kwa ajili ya kugharamia masomo yako.
“Udahili umefunguliwa, nawahimiza vijana kuchangamkia fursa hii. Awali tulikuwa tunawachukua wanafunzi wa kidato cha sita tu, lakini sasa tunawachukua pia mpaka wanafunzi wa kidato cha nne.
“Cha msingi uwe umefaulu vizuri tu, tutakufanyia mchakato wa kwenda kusoma kuanzia ngazi ya diploma (shahada), shahada ya kwanza, shahada ya pili mpaka PhD. “Utaratibu wetu ni mwepesi mno, sisi ndiyo tunakushughulikia kwa kila kitu na tunao uwezo wa kukupeleka kusoma nchini China, India, Malaysia, Uingereza, Australia, Canada, Mauritius na nchi nyingine kibao,” anasema Nick Mussa, Ofisa Habari wa Global Education Link.
“Pia, tofauti na mikopo ya elimu ya juu hapa nchini ambapo anayekopeshwa ni mwanafunzi, sisi tunatoa mkopo kwa mzazi unaoweza kugharamia kuanziaasilimia 50 mpaka 70 ya gharama zote za masomo ya nje na mkopo tunaotoa, hauna riba hata shilingi moja,” aliongeza Nick.
Kuhusu namna ya mwanafunzi anavyoweza kupata nafasi hiyo ya kwenda kusoma nje ya nchi kwa urahisi kiasi hicho, Nick amesema anachotakiwa kufanya mwanafunzi husika kufika kwenye ofisi zao zilizosambaa sehemu mbalimbali nchini.
“Kwa Dar es Salaam, ofisi zetu zipo Chang’ombe mkabala na Kituo cha Mafuta cha Oilcom, jirani na Chuo cha VETA au unaweza kupiga simu ya mezani kwa namba +255 22 285 0889 au simu za mkononi kwa namba 0656 200 200 au 0677 600 100.
“Kwa Arusha ofisi zetu zipo Tanki la Maji mkabala na Hospitali ya Dr Mohamed au unaweza kupiga simu ya mezani namba +255272545774 au kwa simu ya mkononi namba 0782 370 102.
Kwa Mwanza tupo Rock City Mall ghorofa ya pili, Wing A au unaweza kupiga simu namba 0677 500 600. “Jijini Mbeya tunapatikana Mwanjelwa kwenye Jengo la Century Plaza ghorofa ya pili mkabala na Mwanjelwa Complex au tupigie kwa namba 0677 500 800. Dodoma tupo Baseline House ghorofa ya kwanza mkabala na Nyerere Square au unaweza kupiga simu namba 0677 300 700.
“Kwa visiwani Zanzibar, tupo Unguja Mtaa wa Mlandege, Muzzamil Center, Block A ofisi namba 39 iliyopo ghorofa ya tatu au unaweza kutupigia kwa namba 0772 158 158. Tumevuka pia mipaka mpaka nchini Zambia ambapo tuna ofisi yetu jijini Lusaka, Chozi Road au unaweza kutupigia simu namba +260 97 3711178.
“Ukifika kwenye ofisi yetu yoyote kati ya hizo nilizozitaja hapo juu, utapata maelezo ya kutosha na kupewa utaratibu mzima wa namna ya kupata nafasi ya kwenda kusoma ng’ambo na kutimiza ndoto zako.
Tunapeleka wanafunzi wanaosomea masuala ya uhandisi, sayansi, uchumi, biashara, sheria na fani nyingine nyingi, nawasihi wahitimu wa kidato cha nne na cha sita kuchangamkia fursa hii adimu,” anahitimisha Nick.