×

Afcon 2019: Premier Bet Wagawa Zawadi Kibao Bureee! – Video

TIMU ya Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Premier Bet, wikiendi iliyopita iligawa zawadi kwa mashabiki wa soka waliojitokeza katika Ufukwe wa Coco jijini Dar kushuhudia mchezo wa kwanza wa Kundi C wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) kati ya Senegal dhidi ya Taifa Stars.

Katika mchezo huo wa Jumapili usiku, Senegal iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Keita Balde na Krepin Diatta.

Katika kipindi hiki cha michuano ya Afcon inayofanyika nchini Misri, Premier Bet wameanzisha Kampeni ya Mtaa Kwa Mtaa ambayo inalenga kutoa burudani na kutangaza bidhaa zao kwa Watanzania waishio Dar es Salaam.

Kampuni hiyo baada ya kuonyesha mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Senegal, kesho Alhamisi pia itaonyesha mechi ya Taifa Stars dhidi ya Kenya ambapo safari hii itakuwa kwenye kiwanja cha Mikasa kilichopo Ubungo jijini Dar.

Taifa Stars itahitaji ushindi katika mchezo huo kwa kuwa kupoteza kutawatengenezea nafasi kubwa ya kuondolewa kwenye mashindano hayo.

Hitimisho la burudani hiyo ya kuonyesha soka kwenye viwanja vya wazi, itakuwa Julai Mosi, mwaka huu kwenye Viwanja vya Zakhiem vilivyopo Mbagala ambapo siku hiyo Taifa Stars itapambana na Algeria ukiwa ni mchezo wao wa mwisho wa Kundi C.

Miongoni mwa zawadi wanazozitoa ni pamoja na fulana za Premier Bet, wrist bands, Zcards za Afcon, Beer Matt’s na kofia za Premier Bet.

Apostolos Kalodoukas ambaye ni Meneja Mauzo wa Premier Bet, alisema: “Tumeamua kusogeza burudani kwa Watanzania ambao wanapenda kuitazama timu yao na kuonyesha uzalendo, lakini mbali na hivyo tunatumia njia hii kutangaza huduma na bidhaa zetu ambazo zinapatikana kwa njia ya mtandao na kawaida.”

Doris Mtan, Ismail Juma, Selemani Omary, Isack Thomas na Khalid Hassan, ndiyo walijinyakulia zawadi hizo baada ya kushinda bahati nasibu iliyoendeshwa na James Tupa ambaye ni mtu wa masoko sambamba na Sechelela Jonathan, Mariam Muhidini na Salma Nassoro ambao wanatoka kitengo cha huduma kwa wateja.

PICHA ZOTE: ISSA LIPONDA