×

AUNT AFUNGUKA KUMWAGA CHOZI MAHAKAMANI

Staa wa sinema za kibongo, aunt Ezekiel amefungukia chozi lake alilodondosha mahakamani wakati shoga’ke, wema isaac Sepetu akisomewa mashtaka yake. aunt aliliambia gazeti la ijumaa kuwa, alikuwa akiumia mno kila alipokuwa akimtazama wema akiwa amesimama pale kizimbani kwani alijua lolote linaweza kutokea ama kupewa dhamana au kurudishwa mahabusu.

“wema ni rafiki yangu ambaye hata nikiwa na shida kiasi gani anakuwa na mimi wakati wote bila kuchoka hivyo kwa nini nisijisikie vibaya ninapomuona na yeye yupo matatizoni? Roho ilikuwa ikiniuma,” alisema aunt.