×

Salim Aiyee atua KMC Akitokea Mwadui FC

TIMU ya KMC ya jijini Dar, imemsajili Salim Aiyee kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mwadui FC ya mkoani Shinyanga.

 

Aiyee mbali na kusajiliwa na KMC, pia alikuwa akihusishwa na timu nyingi ikiwemo Yanga, Prisons, Azam na JKT Tanzania kutokana na msimu uliopita kufanya vizuri akimaliza na mabao 18 kwenye Ligi Kuu Bara nyuma ya kinara Meddie Kagere wa Simba aliyefunga 23.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, wakala wa mshambuliaji huyo, Ashley Martine, alisema kuwa Aiyee amesajiliwa na KMC baada ya ofa iliyo-kuwa mezani kwao kuwa ngumu kuikataa.

 

“KMC waliwasilisha ofa nzuri ambayo ilikuwa ngumu kwa Aiyee kuikataa ndio maana kasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo,” alisema wakala huyo.

GLOBAL FC Vs BONGO FLEVA: TUNDAMAN Alivyodaka PENALTI Kwa Mbwebwe!