×

Francis Kahata Atua Simba, Jeshi Limekamilika Sasa!

Wakati kukiwa bado kuna sintofahamu juu ya kujiondoa kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Simba ambaye pia ni mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, kama ilivyo ada klabu hiyo kutambulisha mchezaji kila siku katika kipindi hiki cha usajili, leo ni zamu ya Francis Kahata ‘Messi wa Kenya’, ambaye amesajiliwa klabuni hapo kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Klabu ya Gor Mahia.

 

 

Kupitia akaunti yao ya Instagram ya Simba Sc wameandika; Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza eneo la kiungo, kwasasa akiwa sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya kinachoshiriki Afcon, Francis Kahata (27) msimu ujao atavaa jezi ya Mabingwa wa nchi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

@kachikahata amejiunga Msimbazi akitokea Gor Mahia ya Kenya ambapo akiwa kwenye klabu hiyo alishinda Kombe la Ligi Kuu mara tatu, kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya mara mbili na mchezaji bora wa msimu 2018/2019 wa Gor Mahia. #NguvuMoja.